MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA KWA MUDA KUTOCHAPISHWA...

Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.

Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na

MKURUGENZI IDARA YA HABARI

WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

28 SEPTEMBA,2013

MTUHUMIWA WA KIKE ANASWA TENA KWA KOSA LA KUJIUZA, NI BAADA YA KUPEWA MSAMAHA MAALUMU

BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena kwa kosa hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo chake,..

Habari za uhakika zilizopatikana katika Mahakama ya Jiji, Dar es Salaam zinasema kwamba mfungwa huyo alitumikia kifungo chake katika Gereza la Segerea jijini Dar na alipobakiza miezi michache kumaliza alionewa huruma na bibi jela na kutakiwa kumalizia kifungo hicho uraiani.

Inadaiwa kuwa kabla ya kuachiwa, bibi jela alimsihi Blandina kuhakikisha harudii kosa lililompeleka gerezani pindi atakapokuwa akimalizia kifungo chake nje ya gereza.

Blandina akamhakikishia bibi huyo kwamba atakuwa mtu safi kwani amejifunza vya kutosha.

Katika hali ya kushangaza, Jumatano iliyopita Blandina alipandishwa tena katika Mahakama ya Jiji iliyopo Barabara ya Sokoine jijini Dar akiwa amerudia kosa lililompeleka Segerea miezi michache iliyopita.


Imeelezwa mahakamani hapo kwamba, Septemba 24, mwaka huu Blandina na wenzake wanne walinaswa Buguruni usiku wakiwa katika mawindo ya ukahaba.

Bahati mbaya kwa Blandina alipofikishwa mahakamani hapo alikutana na hakimu yuleyule aliyemhukumu kifungo cha miezi sita kwa kosa la ukahaba.


Hakimu huyo, Timothy Lyon alipigwa na butwaa baada ya kumuona Blandina akiwa amesimama mbele yake.


Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na wenzake, Husna Amos, Monica Denis, Esther Chizai na Angela Emmanuel wote kwa pamoja walisomewa mashtaka yao na kukana.

 Hakimu Lyon aliwaambia watuhumiwa hao kwamba dhamana iko wazi na kuwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na shilingi laki mbili.

Sharti hilo lilionekana kuwa gumu kwa watuhumiwa wote, hivyo walipandishwa karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Oktoba 15, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo

PICHA YA MSANII RECHO KATIKA POZI LA NUSU UCHI...

MSANII wa filamu za kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ hivi karibuni aligeuka kituko baada ya kutupia picha ya nusu utupu katika mtandao wa kijamii.

Picha hiyo ambayo Recho amevaa shati tupu (inayoonesha ndani) bila kuvaa kitu kingine chochote, aliitupia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo mashabiki na marafiki zake walichangia huku wakimlaumu kuwa hakufanya vizuri kuiweka picha hiyo ya aibu mtandaoni.

Mwandishi  wetu alimuuliza Recho kulikoni? Akajibu hivi:
“Nawapenda sana marafiki zangu lakini mimi sijaona tatizo la hii picha kwa sababu ni ya kawaida sana sioni ubaya wake.”

KESI YA KUPINGA KODI YA SHILINGI 1000 KWA MWEZI KWA KILA MTANZANIA MWENYE SIMU YAANZA KUSIKILIZWA..

ZIKIWA zimebakia siku mbili kabla ya serikali kuanza kuwatoza kodi ya laini (sim card) watumiaji wa simu, Taasisi ya Watumiaji wa Bidhaa na Huduma imefungua kesi Mahakama Kuu kupinga sheria hiyo.

Taasisi hiyo ya Consumers of Goods and Services Across the Country ilifungua kesi hiyo juzi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura na kuanza kusikilizwa jana mbele ya jopo la majaji watatu.
 
Majaji waliosikiliza kesi hiyo ni Lawrence Kaduri, Aloysius Mujuluzi na Salvatory Bongole.
 
Katika kesi hiyo walalamikaji wanaiomba mahakama itangaze kwamba sheria iliyopitishwa na Bunge inayotaka kila mtumiaji wa simu ya mkononi kukatwa sh 1,000 kila mwezi ni kandamizi.

Walidai kwamba watumiaji wengi wa simu za mkononi hawana uwezo wa kukatwa fedha hiyo kwa mwezi, huku wakisisitiza kuwa itawaathiri watumiaji wa huduma hiyo.
Kwa mujibu wa madai ya walalamikaji hao, sheria hiyo inakiuka matakwa ya katiba ya nchi ya uhuru wa kupashana habari na kuiomba mahakama kuifuta sheria hiyo waliyoiita kuwa kandamizi.
 
Mawakili wa walalamikaji kutoka Kampuni ya uwakili ya Rex, Lugano Mwandamo na Merkizedeki Lutema walidai kuwa wateja wao wanataka mahakama imzuie Waziri wa Fedha kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoza kodi hiyo hadi hapo maombi yao yatakapotolewa uamuzi.
 
“Kuanzia sasa hivi mahakama itoe amri ya muda kuzuia utekelezaji wa sheria hiyo usitendeke,” alidai Mwandamo.
Kutokana na maombi hayo, jopo la majaji liliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 3 mwaka huu, likimtaka wakili wa serikali, Kelley Mwitasi kuwasilisha maelezo yake kwa njia ya maandishi.
 
Wakati huo huo, majaji hao waliutaka upande wa walalamikaji kujibu maelezo ya upande wa serikali kwa njia ya maandishi na kuyawasilisha mahakamani hapo kabla ya Oktoba 7, ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa saa saba mchana siku hiyo.
 
Kufunguliwa kwa kesi hiyo kutasitisha utekelezaji wa utozaji wa kodi hiyo unaotakiwa kuanza Septemba 30 mwaka huu, baada ya TRA kuziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze utekelezaji wa sheria hiyo.
 
Sheria hiyo iliyopingwa na wanasiasa wengi bila kujali itikadi za vyama vyao, ilipitishwa kwa nguvu ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa Bunge la Bajeti na kutaka utekelezaji wake uanze Julai 30.
 
Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya serikali kuu.

Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa hata wa CCM dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.
 
Malalamiko hayo, yalimlazimu Rais Jakaya Kikwete kukutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.
 
“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema rais kwenye kikao hicho.
 
Licha ya agizo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty’ kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, kodi ya laini za simu haijaondolewa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.

Takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.

ZAIDI YA WANAWAKE ELFU 8 NCHINI NIGERIA ,WAANDAMANA KUSHINIKIZA SERIKALI IWASAIDIE WAOLEWE...

Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua. 

Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa. 

Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!) 

Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine. 

Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao. 

MAISHA YA DIAMOND NI AIBU TUPU, MDOGO WAKE AAMUA KUMUUMBUA... MSIKILIZE HAPA

Mdogo  wa  Diamond  ameamua  kumuumbua  kaka  yake.Kayaanika  maisha  yake  yote  tangu  akiwa  underground  hadi  star...

Dodo  anadai Diamond  alikuwa  ni  muuza  supu  ya  ngozi, mswaki  alikuwa  anapiga  mara  moja  kwa  wiki...

Inadaiwa  Diamond  alikuwa  ni  mnywa  Gongo, chokoraa  na  mengine  kibao  ambayo  mdogo  wake  kaamua  kuyaanika....

MSIKILIZE  HAPO  CHINI...

WEMA SEPETU ATIMIZA MIAKA 25 LEO, AJIGAMBA NA KUDAI YEYE BADO NI BINTI MBICHI

Leo mwanadada wema sepetu anaherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 25 toka alipoletwa hapa duniani na wazazi wake mzee Abraham Sepetu na mama Wema..

Mwanadada huyu ambaye kwa sasa yupo hong kong – China amemiminiwa salamu mbalimbali na mastaa wenzake  pamoja na fans wake kupitia  kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii...

Kajala amemwandikia wema:
"To the most beautiful, selfless, giving, and considerate person that I know.Am so luck to av as special friend in my heart&thats why your my ride and die Bff, you represent a very special friendship.

 "One which ought to be preserved and cherished forever. I probably dont tel you enough how much I lov you, but I treasure our friendship soo much my bby& I will always b hear for you as u have always be there for me sweety pie.

"My heart and very being will always hold a very special place for you. And even though I am not there physically to celebrate this special day with you, rest assured that you are in my thoughts.

"Kuwa na hakika siku yako hii inasheherekewa na wengi kwasababu wewe ni mwema na ni mama kwa wengi, HAPPY BIRTHDAY My Darling BEST FRIEND...lots of kisses & cuddle lv u so much"
 

Zamaradi Mketema naye ameandika:
"Kuna mtu muhimu sana KWANGU amezaliwa siku ya leo.. I dont know where to start kiukweli.... i just dont know!!!

"Before anything i wanna thank you for giving me a family, beautiful people wenye mioyo ya kipekee @nsepetu @tsepetu @ssepetu i wish mama was on insta so that i tag her as well... watu ambao wamekuwepo pale kwa ajili yangu muda wote.. but kikubwa kuliko vyote you are an angel to me!!!

"Kwangu wewe ni RAFIKI ambae amevuka hata maana ya neno lenyewe... umegusa maisha yangu katika namna ya kipekee mno.. and i have so many reasons to say that.. When i recall about msiba wa mamaangu.. i cant avoid your face WEMA". 

Toka   jijini Hong Kong, Wema Sepetu  amepost video akiwa na mwanadada aunty ekeziel wakisherehekea siku yake ya kuzaliwa leo..

Unaweza kuitazama video hiyo hapo chini

JOHARI AAMUA KUJIFUNGIA NDANI KUKWEPA AIBU YA FUMANIZI.......

Muigizaji maarufu Blandina Chagula(Johari) anadaiwa kuishi kwa kujificha ficha baada ya hivi karibuni kumshushia makonde muigizaji mwenzake Chuchu Hans ambapo kisa kilidaiwa ni kugombea penzi la Vicent Kigosi(Ray).


Inadaiwa Johari hataki hata kukutana na watu wake wa karibu wakiwemo wasanii wenzake.


Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema  kuwa  kwa sasa Johari hataki kabisa kuonana na watu wake wa karibu, hata mtaani amekuwa haonekani mara kwa mara, anawakwepa hata wasanii wenzake, hii ni kutokana na lile sakata lake na Chuchu...


Nae Johari alipoulizwa na mtandao huo juu ya sababu ya kujifungia ndani alisema: "Niko nyumbani, sitaki kutembea sana kwani niko na likizo fupi, halafu hata hili sakata langu na Chuchu bado halijapoa"

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU SAMANTHA.....MWANAMKE ANAYEDAIWA KUONGOZA SHAMBULIZI LA KIGAIDI NCHINI KENYA HIVI KARIBUNI..!!


TUKIO kubwa la kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika jengo la maduka makubwa na ya bei mbaya jijini Nairobi la Westgate, limeelezwa kuwa liliongozwa na mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite.
Yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua juu yake.

1. Samantha, mwenye umri wa miaka 29, ni mzaliwa wa Buckinghamshire, Uingereza anayeelezewa na magaidi wa kundi la Al Shabaab kama mwanamke mwenye akili nyingi, akiwa ni mama wa watoto watatu ambaye alikata mawasiliano na familia yake baada ya kuhamia Kenya mwaka 2007.
2. Ripoti za kipolisi zinaonesha kuwa ni mkufunzi wa wanawake wa kikundi hicho cha kigaidi wanaochukua mafunzo ya jihad, mke wa zamani wa Germaine Lindsay, ambaye alijiua baada ya kuhusika na shambulio la bomu kwenye treni ya chini ya ardhi jijini London, Julai 7, 2005.
3. Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali zinazoaminika kuwa ni zake, ambazo zilitangazwa na Gazeti la Daily Mail la Uingereza, mwanamke huyo anawalea watoto wake ili waje kuwa wanaharakati wa imani kali. Mumewe wa pili, Habib Saleh Ghani naye ilidaiwa kuwa aliuawa kwenye tukio lingine la ugaidi.
4. Baadhi ya nyaraka zinaonesha kuwa katika baadhi ya mawasiliano na mumewe, aliwahi kusema: “Ghani alizungumza na kijana wangu wa miaka nane na binti yangu wa miaka mitano akiwauliza wanachotaka kuja kufanya wakiwa wakubwa, wana majibu mengi lakini wote wanakubaliana kwamba watakuja kuwa Mujahidina.
5.  Ni mtaalamu wa kutengeneza vifaa vya kuficha sura, pua na kichwa, akiachana na taaluma yake ya zamani ya ubunifu wa mitindo ya mavazi ambayo sasa anashona yanayovaliwa na Waislamu, kazi aliyoianza akiwa chini ya uangalizi wa magaidi hao wakati akiishi Mombasa nchini Kenya.
6. Anahisiwa kuwa ndiye aliyetupa guruneti katika baa iliyokuwa imejaa mashabiki wa soka wakitazama mechi za Euro mwaka 2012 katika mechi kati ya England na Italia nchini Uganda Juni 24 na kuua watu watatu, akiwemo mtoto aliyekuwa na umri wa miaka mitatu. Isack Simiyu, (23), aliyekuwa nje ya Jericho Bar, alisema shambulio hilo lilifanywa na mwanamke wa kizungu aliyejifunga kitambaa cheusi kichwani. Alidai kumuona vizuri mlipuaji huyo na polisi walipompa picha nne za wanawake wa kizungu ili aone kama mlipuaji alikuwa mmojawapo, aliichagua ya Samantha.
7. Ni gaidi wa kike anayetisha zaidi kwa sasa tokea alipoondoka Ulrike Meinhof, mwanzilishi wa Kundi la Red Army ambalo lilihusika na milipuko ya mabomu katika Ujerumani Magharibi kwenye miaka ya 1970.
8. Alipokimbia katika nyumba aliyokuwa amepanga mjini Mombasa, polisi walikuta kitabu kidogo cha kumbukumbu akiwa ameandika kuwa anataka watoto wake waje kuwa wakujitoa mhanga. Pia walikuwa na bunduki za kisasa, risasi, pamoja na mapipa ya kemikali yanayotumiwa na wanaojilipua.
9. Akiwa na jina la Kiislamu la Asmaa Shahidah Bint-Andrews, kijana wake wa kiume, Abdur-Rahman Faheem Jamal, alizaliwa katika Hospitali ya Stoke Mandeville mwaka 2009. Katika cheti cha kuzaliwa cha mwanae, hakuna jina la baba lililoandikwa. Alislimu akiwa na miaka 18, akiachana na uvaaji wa jeans na Tisheti na badala yake akivaa mavazi ya Kiislamu, ikiwemo hijab.
10. Alisoma masomo ya dini na siasa katika shule iitwayo Oriental and African Studies huko Russell Square, London, umbali wa mtupo wa jiwe kutoka pale mumewe alipojiua kwa kujilipua.

AGNESS MASOGANGE AAHIDIWA NDOA MARA ATAKAPOTUA BONGO...!!MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.

Translate